Serikali imetangaza kuondoa video zinazokiuka maadili katika jamii ikiwemo zile za ngono na uchi kwenye mtandao wa Tiktok hapa nchini.
Kauli hii inajiri baada ya kufanya kikao kati ya Rais William Ruto na mmiliki wa
mtandao wa Tiktok Shou Zi Chew Agosti 24,2023.
Katika mkutano wa wawili hao, kiongozi wa Taifa aliafikiana na mmliki
huyo kwamba Tiktok itashirikiana na serikali ya Kenya kudhibiti maudhui ya video na kazi za wasanii zinazosambazwa kwenye mtandao huo ili kuondoa dhana potofu na mtumizi mabaya ya mtandao huo.
Vile vile waliafikiana kuweka mikakati ya kuhakikisha watumiaji wa
Tiktok nchini wanapata kipato kutokana na video wanazosambaza katika
mtandao huo.
Katika juhudi za kulainisha shughuli zake humu nchini, Tiktok ilikubali
kuanzisha ofisi zake hapa nchini na vile vile mataifa mengine barani
afrika.
Mkutano huo ulijiri baada ya rais Ruto kuweka wazi kwamba alifanya
mkutano na wamiliki wa mitandao ya Youtube na Twitter kuhusiana na jinsi
ya kuwezesha wasanii kupata kipato kutokana na kazi zao.