Itawalazimu viongozi kutoka bara afrika kushirikiana kutoa maoni katika kongamano la kujadili mabadiliko ya tabia nchi.
Hii ni kulingana na waziri wa mazingira Soipan Tuya, aliyetaja haja ya nchi za Bara la Afrika kushirikiana ili kukabiliana na tatizo hilo huku akiwapongeza viongozi waliohusika na maandalizi ya kongamano hilo akiwemo Rais William Ruto
Tuya alisema kuwa kongamano hilo linanuwia kufanikisha mipango ya kuboresha mazingira ya nchi za Bara la Afrika ili kuongeza ukuaji wa viwanda kupitia teknolojia na ufadhili wa kutosha.
“Tunapoanza kongamano hili tunatarajia kupata maoni yenu ya jinsi tutakavyobadilisha mtazamo wa nchi za Bara la Afrika katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi , safari hii haijakuwa rahisi ningetaka kuwashukuru viongozi wote waliofanya maandalizi ya kongamano hili.”Alisema Tuya.
Kongamano hilo linatarajiwa kutoa fursa kwa nchi barani Afrika kujiendeleza na mikakati mipya ya kukabiliana na mswala ya mabadiliko ya tabaia nchi.
Wakati huo huo Tuya aliwahimiza wananchi kutilia maanani kongamano hilo la siku tatu na kuja na njia ambazo zitatumika kuwezesha mataifa ya Bara Afrika kukabili athari hizo.
“Kongamano hili litoa fursa kwa mataifa ya Bara Afrika nafasi ya kujiendeleza na kuja na njia mpya zitakazotumika kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi ,nawasihi nyote mtumie siku hizi 3 kujifunza na kutoa maoni ya jinsi gani Bara la Afrika litaweza kukabili atahari hizo.”alisema