Kuna ongezeko la utumizi wa bangi kwa asilimia 90, hii ni kulingana na tafiti iliyofanywa na Mamlaka ya kudhibiti utumizi wa mihadarati na unywaji wa pombe nchini NACADA.
NACADA ilibaini kuwa ongezeko hilo ni la maradufu katika kipindi cha miaka 5, wakitaja kutokana na dhana potovu kuhusu madhara yake ikiongeza kuwa ongezeko hilo ni maradufu katika kipindi cha miaka 5.
Hata hivyo mamlaka hiyo ilisema kwamba kati ya dawa zote za kulevya pombe ndio inayotumika sana humu nchini huku viwango vya juu ikiwa eneo la Magharibi ikifuatiwa kwa karibu na Ukanda wa Pwani.
Mmoja kati ya Wakenya wanane wa umri wa miaka 15 hadi 65 ambao kwa jumla ikiwa ni Wakenya milioni 3.1 kwa sasa wakitumia pombe.
“Mmoja katika kila wanaume 5 wenye umri wa miaka 15-65 (2,511,763) na 1 katika kile wanawake 20 (687,356) wanatumia pombe,” ilisema NACADA.
Haya yanajiri siku chache baada ya NACADA kukanusha kuwepo kwa aina mpya ya dawa ya kulevya ya Fentanly.