HabariNews

Tamu ya Youth Fund vijana wapata Fursa ya Kutabasamu Kutokana na Ujuzi na Uvumbuzi wao, Mombasa

Hazina ya vijana kenya maarufu Youth Fund Kenya iko tayari kuwasaidia vijana wa pwani kuweza kuleta uvumbuzi wao katika biashara ili wapate ajira na kujiendeleza.

Mwenyekiti wa hazina hiyo Fatma Barayan amesema wako tayari kuwawezesha vijana hawa kifedha kwa kuwapa mikopo ili waweze kutimiza ndoto zao.

“hivi sasa tunazidi kuhamasisha na tumepata kwamba Mombasa imeweza kuanza kujitokeza , vijana wamejitokeza ili kupata kufaidika na hivi funds za youth funds” alisema Barayan.

Aidha Barayan amezungumzia ugumu uliokua wakati wa kuomba mikopo na kudokeza kuwa tayari kuna mipangilio iliyowekwa ili kuondoa swala la vijana kusumbuka wanapoomba mikopo hiyo.

“tuko na products tofauti ambazo zinaempower vijana kujitengezea nafasi za kazi ikiwemo ile mikopo ya vikundi, mikopo ya binafsi na mikopo ya kukuza talanta na vipaji na mikopo ya kukuza uchumi wa ukulima na vile vile wa baharia. Innovation ama invention ni part of talent na tuko hapa kusupoti vijana wa pwani kuwawezesha kutimiza ndoto zao” Aliongezea.

Kwa upande wake Mahmood Noor mwanzilishi wa Swahili Pot Hub alipigia upato hafla ya siku tano ya uvumbuzi pwani iliyoanza hii leo kua na manufaa mengi kwa vijana wa pwani na kuwa itazingatia uvumbuzi ,teknolojia ,vijana na talanta na mengine mengi

Wakati huohuo Noor amesema licha ya hafla hiyo kuwaleta pamoja vijana wavumbuzi na wafanyibiashara wa pwani itawaunganisha na wengine kutoka sehemu zengine za nchi.

“Tunataka mwanzo kuangazia pwani mambo ya uvumbuzi, mambo ya teknolojia, mambo ya biashara, mambo ya vijana ambao wanatumia aidha talanta zao ama fikra zao kujiajiri na kuajiri wengine, pia cha msingi ni kuwakutanisha vijana, wafanyibiashara na wavumbuzi wa pwani kuwaunganisha na wale wengine ambao wanatoka Nairobi, wale ambao wako na mashirika ya serikali pamoja na serikali kuu” Alisema Mahmoud

BY EDITORIAL DESK