HabariNews

Wiki ya Ubunifu Pwani: Vijana Wahimizwa kutumia fursa za Ubunifu Kujiimarisha

Ili kukabiliana na visa vya uhalifu na utovu wa usalama vijana eneo la Pwani wametakiwa kukumbatia ubunifu na fursa mbalimbali za kujikuza na kujiendeleza.

Haya yanajiri huku Wiki ya maadhimisho ya Uvumbuzi Pwani ikiendelea, ambapo vijana walihimizwa kuwa mstari wa mbele kuleta mageuzi.

Zeinab Mahmud, Mkurugenzi wa shirika la Twende green eco-cycle amesema hutumia taka za plastiki na pakiti za maziwa katika utengenezaji wa samani.

Amedokeza kuwa tayari wameweza kutengeneza madawati yaliyopelekwa katika shule tofauti hapa Mombasa kwa majaribio na matokeo yamekua ya kuridhisha.

Tunaokota takataka tunazopata kwa mazingira, za plastiki na za pakiti za maziwa tunazisindika. Tunazikatakata na machine tunazi compress na kuwa ubao mkubwa tunaokata na kutengeza fanicha. Tunaona wengi hawezi kugharamikia madawati yale mwngine sisi tunatengeza madawati kupitia recycling ya taka hizi na kuwauzia kwa bei rahisi,” Alisema Zeinab.

Vilevile Zeinab alisema madawati hayo ambayo huyauza kwa bei nafuu hugharimu kima kichache cha fedha na hayawezi kuharibiwa na wadudu ikilinganishwa na madawati mengine ambayo ni ghali na hayadumu.

Madawati yetu tunauza kwa bei rahisi na ziko imara na zinadumu haziwezi kuvunjika rahisi wala kuingiliwa na wadudu kama zile dawati za mbao. Tukiangalia dawati moja kwa shule ni kama elfu 6 au elfu 7 kwa wengine lakini sisi tunauza kwa bei ya chini, shilingi 4,800.” Alisema.

Kwa upande wake Victor Mwendwa ambaye ni Mwenyekiti wa shirika la ‘Takataka ni Mali’ alisema wamebuni mbinu ya utumiaji wa taka za plastiki kwa kutengeneza bidhaa kutumia tekknolojia na mashini ya kisasa.

Tuna teknolojia tofauti tofauti ambazo uvumbuzi wake umefanyika hapa nchini, kunayo inatenganisha plastiki na takataka na kutengeza vyombo vipya kama beseni. Teknolojia ya Echo loop ni mtandao wa kidijitali ambao unabadili taka kuwa bidhaa zingine na hatimaye kuhifadhi mazingira yetu,” alisema.

Haya yanajiri huku maadhimisho ya Wiki ya Uvumbuzi Pwani yakiendelea.

BY MJOMBA RASHID