HabariNews

Wakazi Changamwe watakiwa Kukumbatia Mfumo sasa wa Upishi kuhifadhi na Kupunguza Gharama ya Maisha

Baadhi ya mashirika pamoja na serikali ya kaunti  ya Mombasa wamekuja pamoja kumfikia mkaazi wamashinani katika kampeni inayolenga kupiga vita dhidi mabadiliko ya tabia nchini na kupunguza gharama ya maisha.

Waziri wa maji maliasili na mabadiliko ya tabia nchi kaunti ya Mombasa Emily Achieng,aliwataka wanajamii kukumbati mfumo wa sasa wa upishi safi (Clean Cooking ) kama njia moja wapo ya kuhifadhi mazingira na kuwapunguzia gharama ya juu ya upishi hasa wanapotumia  makaa au bidhaa za mafuta ikiwemo mafua ya taa na gesi.

Ushirikiano huu kati ya serikali ya kaunti ya Mombasa, GIZ  pamoja na  clean cooking association umepigia upato utumizi wa  majiko ya kisasa yanayotumia mbinu salama ya umeme na miale ya jua katika upishi ili kupunguza madhara ya kiafya yanayotokana na utumizi wa bidhaa zinazotoa moshi na mashizi na kushusha gharama za upishi kwa wakaazi mashinani.

 “Tuko hapa tunaeleza wananchi, clean cooking methods zinasaidia kupunguza madhara ya afya ambayo yanatokana namakaa na moshi na mashizi, pia tunaangazia gharama ya kupika, mafuta taa yamepanda, makaa yamepanda na tatu ni katika kuimarisha mazingira na pia tunawaeleza kuhusu upishi wa umeme.unaweza kutumia unit moja kupiga milo mitatu na ukiangalia unit moja ni Sh.26 kwahio itakua bado amesave katika ile gharama.” Alisema Emily.

Kampeni hio iliyofanyika katika ukumbi wa kijamii wa changangamwe, inatarajiwa kufanyika Kauti nzima ikiangazia uhamasishaji kwa wanajamii, kutambua baadhi ya vikundi ambavyo vitapokeamafunzo ya jinsi ya kutengeneza majiko ya kisasa ya jamii (improved community Jiko) na kutoa msaada kupitia kwa hazina teule kusaidia utengenezaji wa majiko hayo yatakayouzwa kwa bei  ya ruzuku.

 “kampeni hii iko na sehemu tatu ambazo zitazunguka kaunti nzima. Sehemu ya kwanza ni kuhamasiha , pili ni kutambua vikundi vitakavyopokea mafunzo hasaa ya kutengeza improved jiko ya community na tatu ni kuwapatia support, kuna hazina ambayo itasaidia vile vikundi kutengeneza ile jiko ili iweze kuunzwa kwa bei ya ruzuku” Aliongezea.

Maxwel Musyoka anafanya kazi na shirika la GIZ katika mradi wa ENDEV (energizing development) kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa kuhakikisha kwamba kila mkenya kufikia mwaka wa 2028 anatumia jiko ambalo ni safi na mafuta safi kwa kiafya na mazingira . Maxwel alitilia mkazo utumizi wa majiko akitoa wito kwa wakaazi kutoa dhana potofu kuwa utumizi wa umeme kupikia ni ghali mno.

 “ Kupika na umeme itakua ni nafuu kuliko kutumia kuni au makaa, haya majiko tunayoyapigia debe kuna yale yanayotumia ethernaol, kuna majiko ambayo yanatumia sola kwahio ukiwa mahali popote Kenya hii Mombasa hii unaweza kuwa na jiko lako” Alisema Maxwel.

Kwaushirikiano na Kaunti na mashirika mbali mbali Maxwel, aliwapa imani wakaazi na wakenya kwa jumla kuwa bei ya majiko haya itakua chini na utumizi wake katika tika masuala mbali mbali ya upishi itakuwa ya gharama  itakayomjali mwananchiwa tabaka la chini. Kina mama na vijana pia waliahidiwa kupata ajira katika utengenezaji wa majiko haya na baadhi wakiwa ikama mawakala wake.

 “ pia kutakua na mafunzo kwa vijana, kina mama kwa ule mradi wa kusema kwamba ‘leave no one behind’ watapata ajira wakijifunza kutengeza kuyatengeza majiko ya clean cooking na pia kuwa kama mawakala wa haya majiko ya umeme” Alisisitiza.

Teknolojia hii ijaniri muda mwafaka wakati aambapo mkaazi wa Mombasa na taabika na gharama ya juu ya mafuta huku mpishi akihitajika kutumia takriban shilingi 150 kugharamikia mapishi  yam lo wa familia yake hasa katika vitongoji vy kauti ya Mombasa.

Ni mapishi ambayo iko portable ,ukiwa na unit moja unaweza kupiga vyakula hata siku nzima ukamaliza. Chombo hiki kimewekwa alama ya one kilo wart ambayo ukitumia kwa lisaa limoja inatosha kupika vyakula ina kadhaa ukitumia labda Sh.26 ama 30 ambayo ni gharama ya unit moja hapa Kenya.”

Alisema Danson Ligare mwanaharakati wa kuhamasisha teknolojia mpa ya mapishi.

BY EDITORIAL DESK