HabariNews

Rais Ruto Akaza Kamba Kuilinda Sondu

Hatimaye rais William Ruto amevunja kimya chake kuhusu ghasia zinazoendelea katika eneo la Sondu.

Kiongozi huyo wa taifa aliagiza vikosi vya walinda usalama kuwakamata wahusika wote wa ghasia katika eneo hilo huku akitoa onyo kali kwa wanasiasa wanaochochea wakaazi wa Sondu kushikriki katika mapigano ya kikabila.

Akizungumza katika kaunti ya Kisumu Rais Ruto alisema kuwa uchunguzi unaendelea na kwamba mkono wa sheria hautamsaza yoyote atakayepatikana na hatia.

Kuna watu wanaturudisha nyuma na kuleta vita kati ya jamii na kati ya majirani.Nishamwambia prof Kithure Kindiki vile tumewakabili magaidi kule Northrift na wanamgamboa wa Al Shabab, hawa watu wa Sondu hapa watakiona cha mtema kuni,”rais alidokeza.

Katika zuara yake rasmi ya siku tatu ya eneo la Nyanza amabalo ni ngome ya mrengo wa upinzani Oktoba 06, rais aliwataka viongozi wa eneo hilo kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuyapa kipaomnbbele masuala ya maendeleo.

Mimi nitarudi hapa Jumatatu nitazunguka hapa mpaka mnizoee na mimi pia niwazoee.Si tumekubaliana mambo ya siasa tulimaliza, gavana si ni huyu Orengo na rais ndio mimi hapa. Sasa deni ambalo tuko nalo kwenu ni deni la Maendeleo,” rais alieleza.

Ikumbukwe kwamba Oktoba 05, waziri wa usalama na masuala ya ndani Prof Kithure KIndiki aliwahamisha maafisa wa usalama katika maeneo hayo yanayokabiliwa na utata wa kiusalama huku akiahidi kwamba iwapo itabainika kwamba baadhi ya walinda usalama walihusika kati.

BY MWAJUBA.