HabariNews

Rais William Ruto Apitisha Mswada wa Ubinafsishaji wa Mashirika ya Serikali

Rais Ruto amepitisha mswada wa ubinafsishwaji mashirika ya kiserikali yasiokwa nafaida

Rais Ruto alitia sahihi mswada huo  kwa minaajili ya kurahisisha shuguli za ubinafsishaji wa mashirika ya serikali yasiyo na faida ili kupunguza mzigo wa gharama kwa serikali huku akimvika jukumu la utekelezaji wa sheria hiyo Rebecca Miano ambaye ni waziri wa biashara na viwanda

Sheria hiyo ilipendekeza kubuniwa kwa mamlaka ya  ubinafsishaji huku shughuli za ubinafsishaji zikitarajiwa kuanza kwa kupitia kwa waziri anaehusika na shirika hilo ambaye atawasilisha pendekezo lake kwa baraza la mawaziri na kisha kupelekwa bungeni kabla ya kukabidhiwa mamlaka ya ubinafsishsaji.

Kuuza hisa za mashirika hayo kwa wawekezaji binafsi ulitajwa kua moja ya mbinu zitakazo tumiwa kwenye kubinafsisha mashirika hayo.

 BY EDITORIAL DESK