HabariNews

Takriban Wanafunzi 26,000 wanahofiwa kukosa HELB Mwaka huu

ZAIDI ya wanafunzi 26,000 watakosa kupokea ufadhili wa serikali baada ya kujiunga na vyuo vikuu na Vyuo vya Mafunzo ya Kiufundi (TVET).

Hali hii imezua hofu miongoni mwa wazazi, ya gharama ya juu ya masomo kwa baadhi ya watoto wanaotarajiwa kuiunga navyuo hio ikizingatia kuwa waliotuma maombi pekee ndio watakaofuzu kupokea ufadhili na mikopo ya elimu.

Oktoba 7, 2023 ilikuwa Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi hayo, muda ambao uliongezwa kwa mwezi mmoja kufuatia idadi chache ya waliotuma maombi na takriban nusu ya wanafunzi kufungiwa nje mwezi Septemba.

Ingawa tarehe ya mwisho ya kutuma maombi kwanza ilikuwa Septemba 7, 2023, muda uliongezwa hadi Oktoba 7, 2023, ili kuwaruhusu wanafunzi wote waliofuzu kuwasilisha stakabadhi zao kwa lengo la kutomwacha nyuma mwanafunzi yeyote,” alisema Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu kupitia taarifa.

Kufikia Oktoba 4, 2023, hata hivyo, ni jumla ya maombi 238, 714 yaliyokuwa yamewasilishwa.

Wanafunzi jumla ya 269,112 waliteuliwa na Huduma ya Uteuzi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Mafunzo Nchini (KUCCPS) kujiunga na vyuo vikuu na taasisi za Tvet na walifuzu kupokea ufadhili wa serikali.

Hata hivyo, wanafunzi 3,608 na 26,790 walioteuliwa kujiunga na vyuo vikuu na Tvet bado hawajatuma maombi.

Idadi hii inatarajiwa kuongezeka baada ya huduma ya uteuzi kuthibitisha data ya wanafunzi ambao wamehamia kozi mbalimbali za digrii na vyuo vikuu,” alisema.

Hazina ya Vyuo Vikuu na Bodi ya Mikopo kuhusu Elimu ya Juu (HELB) zimeanza mchakato wa kutoa ufadhili wa elimu na basari kwa wanafunzi wote.

Kulingana na Mfumo wa Kipimo cha Jumla utakaoainisha wanafunzi wa KCSE, wale maskini ni wanaotoka kwenye familia zenye mapato kati ya Sh23,672 na Sh70,000 kila mwezi huku familia za wanaojiweza zikiwa na mapato kati ya Sh70,001 na Sh200,000 kila mwezi.

BY EDITORIAL DESK