Idadi ya watu wanaougua Ugonjwa wa Utandu wa macho (Eye Cataract) yaripotiwa kuongezeka huko kaunti ya Kwale.
Wataalam wa macho walitaja baadhi ya sababu zilizopelekea ongezeko la visa vya wanaougua ugonjwa huo ikiwemo uzee pamoja na watoto wanaozaliwa nao.
Kulingana na msimamzi wa hospitali ya Kwale eye Centre (Magandia), Verena Ndunda, idadi ya wanaotembelea hospitali hiyo iliongezeka ikilinganishwa na hapo awali. Ndunda alibaini kuwepo haja ya wakazi kujitokeza mapema wakiwa watoto au watu wazima kukaguliwa macho ili kuepukana na madhara zaidi yanayosababishwa na kufika hospitalini kuchelewa.
“Ugonjwa ambayo tunaweza sema umekithiri kwa upande huu wa Kwale ni Utandu, lakini siku hizi tunapata changamoto kwa upande wa kupimwa miwani, watu wengi wankua na changamoto hii ambapo inabidi wapimishwe miwani iweze kuwasaidia kuona. Kwa upande wa macho ukisikia unasikia vibbaya kwa macho nenda hospitali ukaonekane, hio mambo ya majani haitakikani, unaweza ukaharibu macho zaidi kwahivyo kama unashida ya macho utembelee kituo uonekane na wataalamu wenyewe.” Alisema Ndunda
Daktari Shabir Abdulrasul ambaye ni mtaalamu mkubwa wa upasuaji wa macho katika hospitali hiyo aidha, aliwataka wakaazi kusaka matibabu mapema badala ya kutumia dawa za mitishamba ambazo mara nyingi zinaleta madhara Zaidi.
“ ile upasuaji tunafanya mingi kabisa ni ya Utandu. Utandu kuna aina tofauti, kuna zile mtoto anaweza zaliwa nayo, kuna zile unaweza pata wakati jicho limeumia inaweza kua mtoto, mtu mzima , kuna utandu wa ugonjwa wa sukari kisha kuna utandu ile ya kwaida ya uzee. Mwanzoni utandu ulionekana baada ya miaka 70, siku hivi vile maisha imebailika tumeanza kuona utandu mapema kidogo mpaka miaka 50 tumeona utandu ya uzee imeanza kuingia” Alielezea Dr. Shabir
Kufikia sasa hospital hiyo ya macho ina uwezo kuwahudumia zaidi ya wagonjwa 130 kwa siku ikilinganishwa na idadi ya hapo awali.