HabariNews

Taka Ni Mali! Kaunti ya Kilifi Yaonya vikali Utupaji Taka Ovyo ovyo

Serikali ya Kaunti ya Kilifi imetenga sehemu maalum ambazo zitatumiwa kutupa taka ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

Waziri wa mazingira na maji katika kaunti hiyo Omar Said aliyathibitisha haya akisema kuwa magari ya kubeba taka yamesambazwa katika sehumu tofauti kubeba taka hizo na kuzipeleka sehemu moja.

Katika mahojiano ya kipekee Said aliwaonya wananchi katika kaunti hiyo dhidhi ya kuanzisha sehemu za kutupa taka ambazo hazijaidhinishwa rasmi na serikali hiyo akisema watakaopatikana watachukuliwa hatua za kisheria.

Kuna sehemu nyingi zisizosahihi zinazotupwa taka na ambazo zimeanzishwa na wananchi wet. Kuna pahali ambapo tumetenga kama serikali na tuko na mipango ya magari yetu ya serikali kupitia sehemu hizo ibebe taka hizo kufikisha katika sehemu za taka zilizotegwana kauti “ AlisemaSaid

Said Vile vile alitoa ushauri kwa vijana walio katika makundi kusaidia serikali hiyo katika utunzaji mazingira akisema hatua hiyo inabuni nafasi za ajira kwa vijana.

Umuhimu wa kushirikiana na hizi CBOs ni kwanza chanzo cha ajira kwa vijana wengi ambao ni wa mtaa huu ama eneo hili, kwa sababu taka ni mali. Tunataka wajitokeze kufika maeneo yote ya kaunti ya Kilifi kwa ujumla ” Aliongezea

BY JOSEPH JIRRA