Ni afueni kwa Wakazi waliokuwa wakiishi katika makazi ya Buxton baada ya Rais William Ruto kuwakikishia kuwa hakuna mkaazi yeyote atakayeachwa nje ya mpango wa kupata makazi ya kisasa ya bei nafuu.Haya ni baada ya wakazi wengi wenye kipato cha chini na waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo kuibua hofu ya kukosa kupata nyumba kutokana na kipato chao kidogo.
Akizungumza Alhamisi Novemba 2, wakati wa uzinduzi wa Awamu ya pili ya mradi wa Nyumba za Buxton Point, eneo la Mzizima rais Ruto alitoa hakikisho hilo akisema kuwa kupitia sheria ya bunge ya hazina nyumba za makazi iliyopitishwa bungeni, hata wakazi wenye kipato cha chini watapata fursa ya kumiliki nyumba.
Kulingana na rais wakazi waliokuwa wakiishi maeneo hayo ya Buxton watazingatiwa wote na kuhakikisha wanapata nyumba hizo watakazozilipia kwa malipo ya mdogo mdogo kwa muda wa miaka watakayopewa.
“Wakati nyumba hii ilivyo jengwa wale walikuwa hapa ikakuwa hawawezi kufikia malipo ya haya manyumba tena, kukatokea utata, na ndio nimefika hapa kuwaambia leo ya kwamba wale waliokuwa wanaishi hapa nimefika kuwatangazia ya kwamba na nyinyi pia mutapata nafasi ya kuishi mahali hapa. Tumepitisha sheria bunge ya housing fund ambayo itatuwezesha kama serikali kuwa na hazina ambayo itamuwezesha mwananchi wa kawaida apate tenant purchase scheme,” alisema Rais
Wakati huo huo rais Ruto alimtaka gavana wa kaunti hiyo Abdulswamad Sharif Nassir kuhakikisha kwamba mpango wa ujenzi wa nyumba za makazi ya bei nafuu unaoana na mpango wa serikali yake ili wananchi wa kawaida wanufaike vilivyo na makazi hayo kwa malipo ya kadri ya uwezo wao.
“ Mpango wako wa kaunti ilingane na program yetu ya affordable housing kwa sababu ile ya mbele ilikuwa inashughulika na watu wenye mapato ya juu peke yao. Mimi nimekuambia gavana kama mpago ya kaunti haita uzisha mahasla wa chini, kama hakuna nyumba ya shilingi elfu tatu ya mama mboga ama mtu wa bodaboda aweze kulipia aweze kulipia aishi hio program mimi sitakkuwa ndani yake.” Alisisitiza
Rais vile vile aliwaahidi wakazi wa shamba la Kwa Bullo kuwa serikali italeta masoroveya kupima ardhi hiyo na kuhakikisha kuwa wanapimiwa na kupewa hati miliki za ardhi hiyo.
“Pale kwa Bulo tuko na ekari elfu moja, wananchi wamejaa lakini ilikuwa ni shamba ya serikali , ilikua na shamba ya kampuni fulani, tunafanya planning na mimi nataka niwahakikishie ya kwamba hio ardhi tutaifanyia usorovea na mimi nitarudi hapa kuhakikisha ya kwamba kil mwananchi pale Kwa Bulo iyo sehemu yote wanapata hati yao miliki ya mashamba yao,” aliongezea rais Ruto.
Kwa upande wake Gavana wa Mombasa Abdulswamaad Sharif Nasser hata hivyo aliwahakikishia wakazi wa baadhi ya maeneo yakiwemo Khadija, Likoni,Tudor na Changamwe kujumuishwa katika mchakato mzima wa umiliki wa nyumba hizo na kupata nyumba hizo kama walivyoahidiwa hapo awali.
“Na maeneo yote zile project ambazo kwamba kaunti inataka kufanya, we will work hand in hand with affordable housinh policy iliwatu wetu waweze kufaidi katika nyumba ambazo zitakuwa ni raslimali” Alisema Nassir