Wito umetolewa kwa serikali kuangazia maslahi ya watu wanaoishi na ulemavu ili kuwawezesha kunufaika kikamilifu na mipango ya maendeleo.
Kwa mujibu wa Mkereketwa wa masuala ya walemavu kaunti ya Mombasa Josphat Musungu ni kuwa watu wanaoishi na walemavu wamekuwa wakipitia changamoto nyingi kutokana na kupuuzwa kwa masuala yanayowaathiri.
Aidha amelalamikia suala la kubaguliwa na kutengwa katika nafasi za ajira na uongozi nchini akidai wengi hugeukia mbinu za kifisadi kunyakua nafasi walizotengewa kinyume cha sheria.
“ Japo katiba yrtu imejaribu kukuja na vipengele ambavyo ifaa serikali ifuatizie ilikuhakikisha imepeana huduma safi katika walemavu,bado serikai haijafikia malengo yake kikatiba. Utapata mashirika mengi ya kiserikali hayajaajiri hata mlemavu na yale yalioajiri hata asilimia mbili haijafika” Alisema Musungu
kadhalika alieleza masaibu yanayowakumba katika harakati ya kutafuta huduma za kiserikali akisema kuwa majengo mengi ya kiserikali humu nchini yamekosa miundo mwafaka ya watu wa aina hiyo kufikia afisi hizo.
Alitoa wito kwa serikali kukarabati majengo hayo ili kuwarahishia kupata huduma hizo pamoja na kuyapa kipau mbele masuala yanayowaathiri.
“Ningeliomba serikali majengo yote katika taifa la Kenya aidha yawekwe rampu ama lifti sababu ukiweka zile ngazi zinatatiza walemavuwengi kufikia hizo afisi zinazotoa huduma muhimu sana ambazo walemavu wangependa kunufaika na huduma za serikali” Alisisitiza