Baadhi ya wakaazi wa eneo bunge la kaloleni Kaunti ya Kilifi wameeleza kutoridhishwa na kitendo cha mbunge wa eneo hilo Paul Katana kuwachukulia hatua wapiga kura wanne waliomtaka kujitokeza na kuzungumzia tabia za mapenzi ya jinsia moja yanayodaiwa kuendelea sehemu hiyo.
Hii ni baada ya wanne hao kuitwa na idara ya upelelezi kuandikisha taarifa baada ya mbunge huyo kuwashtaki kwa madai ya kumharibia Jina.
Kwa mda wa majuma mawili kumekuwa na vita vya maneno katika mitandao ya kijamii baada ya baadhi ya vijana kudai kulikuwepo na visa vya mapenzi ya jinsia moja katika ofisi ya mbunge wa eneo hilo Paul Katana, na kumtaka kujitokeza ili kuangazia swala hilo.
Inasemakama Mbunge huyo badala yake alichukua hatua ya kuelekea kwa makao ya DCI.
Akizungumza baada ya vijana hao kuandikisha taarifa na DCI, Steven Gharama Mkaazi wa kaloleni alikosoa hatua ya Mbunge Huyo, na kumtaka kuzungumza na wapiga kura wake iwapo wangehitaji ufafanuzi badala ya kuwachukulia hatua.
“Baadhi ya wale ambao wako mamlakani hawayatilii maanani haya mambo ya kuwa vijana wamejitokeza kulaani hilo jambo na baada ya kujua litatatuliwa namna gani wao wanaanza kutishwa. Mimi nataka kuambia vijana muko na babazenu ngangari hamtatishika, kama ni kuenda kotini tunao uwezo wa kuwachukulia mawakili kaloleni si ya mtu mmoja.” Alisema Gharama
Kitsao Ngoa mkaazi wa eno hilo vile vile aliunga mkono kauli ya Gharama akisistiza kuwa mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na maadili ya jamii ya Mijikenda na nisharti liangaziwe kwa makini.
“MCA wa Mariakani alipoambiwa kuna tatizo hili alichukua hatua ya kukaa nao nakuliangazia, sisi pia tukamuomba mbunge achukue hatua hio hio awatafute lakini cha kustaajabisha, mbunge anakimbia kwa DCI. Sisi tunacholilia ni mapenzi ya jisia moja yaishe Kaloleni” Aliongezea Ngoa
Kulingana na maxwel Khonde ambaye ni mkaazi wa mariakani katika Kaunti ya Kilifi, ni wazi kuwa mapenzi ya jinsia moja yameanza kudhihirika wazi katika eneo bunge la Kaloleni nani sharti viongozi watafute suluhu na mapema ili kulikabili kwa wakati ufaao.
“Kumekuwa na tatizo la mapenzi ya jinsia moja katika eneo la Kaloleni Sub county, ni jambo ambalo linaendelea na liko wazi kabisa jamii inalia” Alisema Maxwel