Serikali imesema imeweka makakati kabambe kufanikisha mchakato wa ujenzi wa nyumba
za bei nafuu kaunti ya Mombasa na Pwani kwa ujumla.
Akizungumza na wanahabari hapa Mombasa baada ya kikao na wadau husika, naibu kamishna wa
kaunti ya Mombasa Ronald Muiwawi alipigia upatu mradi wa ujenzi wa nyumba nafuu nchini akisema
utawasaidia wengi kupata makaazi yaliyobora kwa bei nafuu pamoja na kubuni nafasi za ajira.
Aidha alidokeza kuwa serikali imetambua sehemu kadhaa za kutekeleza miradi hiyo katika eneo la
pwani huku wakilenga kupata nyumba 50,000 eneo hilo pindi itakapokamilika.
“Tunalenga kujenga nyumba 50,000 kaunti hii ya Mombasa na tunatarajia kila kitu kitaenda kwa utaratibu
na kwamaba haya yote ambayo yameratibiwa yatakamilika na tunaomba wananchi na viongozi wa Mombasa
washirikiane na kamati husika na serikali kuu kuhakikisha mambo haya yanafanikishwa.Alisema Muiwawi.
Kwa upande wake John Karanja mkurugenzi wa mradi huo ukanda wa pwani ameweka wazi kuwa serikali
imekamilisha mchakato wa kuwafidia waliokuwa wakiishi eneo la Buxton.
Karanja alitoa hakikisho kuwa serikali imeweka mipango ya kuhakikisha wakaazi na wafanyabiashara wa kaunti
ambazo miradi hii inaendelezwa wamenufaika kikamilifu na suala hilo huku akihimiza wananchi kushirikiana na
viongozi kufanikisha hayo. “ili kuhakikisha kila mtu anafaidika na mradi huu umeorodhesha zaidi ya vifa 80,00
vitakavyohitajika na kuhakikisha kila mmoja anafaidi tumekuja na mradi wa kuandikisha wanajauakali, mafundi
na wengine wote watakaohusika na usambazaji wa vifaa hivi.” Alisema Karanja
Naye Suleiman Mwatsanga mkuu wa muungano wa wanajuakali eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa
alipongeza mradi huo akisema utaimarisha maisha ya wengi kwa kuwawezesha kupata ajira na kukimu mahitaji yao.
“Kuja kwa ujenzi wa hizi nyumba kwa sababu watu wa jua kali wamewekwa kando wamedharauliwa hawatambuliki
kwa sababu hawana makaratasi,kazi zao hazina thamani lakini kwa sasa tunashuruku rais William Ruto kuleta hili
jambo na sekta ya hii itawafanya vijana wengi kujishughulisha na kukuza familia zao.” Alisema Mwatsanga.
By MEDZA MDOE