HabariNews

Zaidi ya visa 90,000 vya TB Kifua Kikuu vyarekodiwa nchini Kenya mwaka 2022 Hofu kuu ikisalia Vijijini.

Taifa la Kenya limerekodi ongezeko la idadi kubwa ya wanaougwa maradhi ya kifua kikuu katika kipindi cha mwaka wa 2022 ikilinganishwa na mwaka 2021.

Ripoti na Mpango mkakati ya mwaka 2023/24 imefichua kuwa Kenya imenakili wagonjwa 90,841 kutoka 77,854 katika kipindi cha mwaka wa 2021.

Kulingana na katibu mkuu wa idara ya afya Mary Muthoni Muriuki ugonjwa wa kifua kikuu ni hatari zaidi katika maisha ya Wakenya kutokana na hofu kwamba asilimia kubwa ya waathiri mashinani hawajapata tiba wala hata vipimo ambapo zaidi ya kesi 756 zilikosa tiba baada ya dawa kushindwa kufanya mwili mwao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Wizara ya Afya ya mwaka 2023/24 – 2027/2028 Katibu huyo ameeleza kuwa idadi hiyo inaashiria asilimia 68 pekee ambayo ni kesi 133,000 na kuacha asilimia 32 bila matibabu au hata vipimo.

Muthoni ameeleza kuwa mpango huo ni muhimu katika safari ya kukabiliana na kupumbukuza makali ya ugonjwa huo ambapo kulingana naye wengi wanafariki kutoka na kukosa kufanyiwa vipimo.

takwimu zinasikitisha, inaashiria kuwa 68% tu ya makadirio ya kesi 133,000 za TB ambazo zingeweza kuibuka mwaka huo, na kuacha 32% bila kutambuliwa na bila kutibiwa. Kuibuka kwa wagonjwa sugu wa TB wa dawa, jumla ya 756 katika kipindi hicho, kunaonyesha hitaji la dharura la mwitikio wa kina na ulioratibiwa.” Alisema Katibu

Kadhalika ripoti kutoka kwa shirika la afya duniani WHO inaarifu kuwa watu milioni 10.6 waliugua Kifua Kikuu katika kipindi cha mwaka 2022 ulimwenguni, huku milioni 1.25 wakiwa watoto na vijana waliofikia kubaleghe na kupelekea vifo vya watu milioni 1.1 waliofariki kutokana na makali ya ugonjwa huo.

Wakati uo huo ripoti hiyo imefichua kuwa Kenya ilibainika kuwa miongoni mwa mataifa 30 duniani yaliyo na viwango vya juu vya maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu ambapo zaidi ya watu laki moja elfu 30 wanapata ugonjwa huo kila mwaka.

Dr. Abdourahmane Diallo ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO nchini Kenya.

Kenya, ilitambuliwa miongoni mwa nchi 30 zinazoongoza kwa TB na HIV, shirika la WHO, lilibaini kuwa watu 128,000 wanaugua TB, ugonjwa uliosababisha vifo 17,000 mwaka 2022,” Dk Abdourahmane Diallo, mwakilishi wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa nchini Kenya alisema.

 MJOMBA RASHID