Wakaguzi wa bodi ya bidhaa za kudhibiti wadudu wanasema wamenasa shehena ya dawa bandia za wadudu katika eneo la Lunga Lunga kaunti ya Kwale.
Wakiongozwa na meneja wa idara ya dawa za kudhibiti wadudu ukanda wa Pwani Stanley Nganga, maafisa hao wamenasa makasha hayo haramu ni ya kilo 230 ya dawa aina ya Malex ambayo hayakuwa na kibali cha kuingia nchini.
Meneja huyo aidha anadai dawa hizo haramu zilisafirishwa kwa lori kutoka taifa la Afrika Kusini na kuingizwa nchini kinyume na sheria, na sasa ametoa wito kwa umma kushirikiana na maafisa wake kufanikisha walanguzi hao haramu wa dawa hizo kukamatwa.
Wamesema Masaduku 74 ya dawa hizo hugharamiu zaidi ya laki mbili pesa taslimu hali ambayo huenda inachangia ulanguzi wa dawa hizo humu nchini kwani tayari imebainika ni biashara ambayo imekuwa ikiendeshwa na shirika moja nchini.
Itakumbukwa kuwa kunaswa kwa shehena hiyo kunajiri wiki mbili tu baada ya shehena jingine la dawa hizo haramu kunaswa katika kasha moja la MICT katika kituo cha Freight hapa mjini Mombasa.
BY EDITORIAL DESK