HabariNews

Jackie Maribe aponea; Korti yamwondolea mashtaka ya mauaji ya Monica Kimani

 Mahakama kuu imempata Joseph Irungu maarufu ‘Jowie’ na hatia ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

 Kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani humo, Jaji Grace Nzioka mnamo Ijumaa alisema kuwa mahakama ilishawishika kuwa ni wazi Jowie alitekeleza mauaji ya mfanyabiashara huyo mnamo mwaka 2018.

“Kwa kuzingatia ushahidi kuhusu suala hii mahakama imebaini kuwa upande wa mashtaka umewasilisha ushahidi wa kutosha na umekidhi vigezo…hivyo ni ubainifu wa mahakama hii kwamba mshukiwa wa kwanza alimwua mwendazake,” aliamua Jaji Nzioka.

Hata hivyo ni afueni kwa aliyekuwa Mwanahabari Jackie Maribe baada ya mahakama kumwondolea mashtaka hayo ya mauaji ya mfanyabiashara huyo.

Mapema leo mahakama hiyo imeanza kutoa uamuzi wake kuhusu mashtaka dhidi ya wawili hao aliyekuwa mwanahabari jackie maribe na aliyekuwa mpenzi wake joseph irungu baada ya kushtakiwa kwa mauaji ya mfanyibiashara monica kimani miaka sita iliyopita.

Hata hivyo mashtaka mengine mawili yanayoambatana na kesi hiyo yatatolewa uamuzi mwezi machi makwa huu.

 BY NEWSDESK