Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yamemshtaki naibu rais Rigathi Gachagua kufuatia matamshi yake dhidi ya Jaji wa mahakama Kuu, Esther Maina.
Ikiwa ni mwezi mmoja tangu Naibu wa Rais kufutilia mbali mpango wake wa kutaka kumfungulia kesi jaji huyo wa mahakama Kuu, Shirika la Haki za Kibinadamu nchini KHRC na MUHURI sasa yanamshinikiza aombe msamaha.
Katika kesi walioiwasilisha kortini mashirika hayo mawili ya kutetea haki yanadai kuwa mpango aliokuwa amenuia kuutekeleza naibu wa rais dhidi ya kumshtaki jaji huyo iliweka Serikali Kuu katika hali ya dhihaka na aibu.
Aidha wamedai kuwa endapo mwenendo unaolalamikiwa hautazuiliwa na mahakama basi kuna uwezekano mkubwa wa kutokea machafuko ya kikatiba ambapo wananchi watapoteza imani na Mahakama.
BY NEWSDESK