HabariNews

KIFWA Yatishia Kuelekea Mahakamani Iwapo Sudan Kusini Haitaistisha Ushuru wa Dola

Chama cha mawakala wa mizigo nchini KIFWA kinatisihia kuelekea mahakamani iwapo serikali ya Sudan Kusini itaendelea kutoza dola 350 kupitia kwa bandari ya Mombasa badala ya mpaka wa mataifa haya mawili.

Kwenye kikao na wanahabari viongozi wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Roy Mwanthi wameitaka serikali ya Kenya kuingilia kati na kuhakikisha Suala hili linatatuliwa kutokana na msongamano wa mizigo unaosababishwa na makasha ya mizigo katika maeneo ya Mombasa.

Aidha wamesema chama hicho hakipingi hatua hiyo ya serikali ya Sudan Kusini wakitaka shughuli hiyo kutekelezwa kwenye mipaka ya mataifa haya mawili.
“Serikali ya Sudani imetoa agizo la kwamba kila mzigo unaotoka bandari ya Mombasa illipe dola 350 na hii notisi imetoka hawataki hii pesa ichukuliwe kwenye mpaka wa kuingia Sudan wanataka hii pesa ilipwe kwa akaunti Fulani hapa Mombasa sisi kama mawakala tunauliza kama hii ni ushuru mbona isichukuliwe huko tukipiga simu kuuliza mawakala wa Sudani wanasema hata hao hawajui hii pesa inalipiwa nini.” Alisema Mwanthi.

Hata hivyo mawaka hao wametaka serikali ya Sudan kufahamisha mawakala wa nchini humo kuhusiana na matozo hayo wakisisitiza kuwa mawaka wa kenya hawawezi kulipa fedha hizo wakiwataka wasafirishaji wa mizigo kuchukua hatua kali iwapo mizigo yao itacheleweshwa kutokana na jambo hilo.

“Sisi hatuwezi kulipa hio pesa wachukue hio pesa kwenye mpaka wao ama wafahamishe vizuri wale mawakala wa Sudani watutumie hio pesa tuwalipie, lakini sisi hatuwezi kutoa pesa mifukoni mwetu tukawalipia.” Aliongeza Mwanthi.

Serikali ya taifa hilo imechukua kandarasi ya kusimamia shughuli hiyo kupitia bandari ya Mombasa.
BY MEDZA MDOE