HabariNews

Uzinduzi wa Chama cha Ushirika kunufaisha Akina Mama Mombasa, asema Mshauri wa Rais Karisa Nzai

Zaidi ya kina mama 600 kutoka Kaunti ya Mombasa sasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya Serikali ya Kenya Kwanza kuzindua mpango wa kuwafungulia chama cha ushirika kitakachowapa nafuu kiuchumi kwani kupitia chama hicho wataweza kupata zabuni, mikopo na kazi kutoka serikalini.

Akizungumza na meza yetu ya habari wakati Wa muktano Wa faragha Na kinamama Mombasa, mashauri Wa maswala ya kisiasa katika ofisi ya rais Karisa Nzai amesema kuwa Kenya Kwanza sasa umerudi mashinani kukomboa Kina mama waliokuwa wakikampeni kuwainua.

Nzai kadhalika aliongeza kuwa tayari serikali imeweka mipango kabambe kuhakikishia kuwa vyama hivyo vitakiwa vya maana Kwa Kina mama hususan kibiashara kwani kabla kupata mgao Wa fedha serikali itatoa mafunzo maalumu Kwa Kina mama Hao.

“Tumeanza na kina mama 600 na tumepanga mpango na wale viongozi wenzangu ambao wako kwenye serikali tuone jinsi tutaboresha kina mama hawa,zile nafasi za kazi kina mama walikuwa wanataka kuchukua kule kilindi na kwengine kote tutaomba wakubwa wawasaidie hawa kina mama.” Alisema Nzai

Kwa upande wao kina mama walionufaika na mpango huo wakiongozwa na Nuru Juma naye mama Warda Ahmed walipongeza mpango huo wakiutaja kuwasaidia pakubwa katika kuwawezesha kina mama wenye miradi kupata hazina za serikali katika juhudi za kuwawezesha kina mama kujiendeleza.

“Tunaotoa pongezi kubwa kwa serikali kuwakumbuka kina mama ambao tuna miradi na tutaiendeleza,walitoa ahadi zake kuwa atakumbuka wale wananchi walioko chini tumeona saa hizi wameanza kufanya kazi kama ilivyo kwenye manifesto yao.” Walisema kina mama hao

Mradi Huo unalenga kufikia Kina kutoka maeneo Bunge 290 nchini ukianza Na kaunti ya Mombasa.

BY DAVID OTIENO