News

Asilimia 90 ya waendeshaji bodaboda Kilifi hawana leseni

Asilimia tisini ya wahudumu katika sekta ya bodaboda katika kaunti ya Kilifi wamebainika kukosa leseni za kuendesha biashara hiyo.

Lakini sasa wahudumu hao huenda wakanufaika na mpango wa serikali kutoa mafundisho ya usalama barabarani  na kupata vibali vya kuendesha pikipiki ili kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikikithiri kila wakati.

Kulingana na mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda kaunti ya Kilfi Katambo Hamisi ni kuwa mpango huo unatarajiwa kuanza mwezi huu kwa waendeshaji wote wa pikipiki huku wakitakiwa kulipa shilingi 750 baada ya mafundisho hayo ili kugharamia leseni hizo.

Aidha hatua hiyo ya serikali huenda ikakumbwa na changamoto kufuatia wahudumu hao wa bodaboda kuitaka serikali kuwapa marupurupu wakati wa mafundisho hayo.

Wamesema hatua hiyo ya kulipa shilingi mia saba na hamsini ili kupata leseni hiyo haitakuwa rahisi  kwao wakisema kwa sasa wanapata pesa ya kununua chakula pekeyake.

Comment here