Habari

ASK yaomboleza

Chama cha maonyesho ya kilimo humu nchini ASK tawi la Mombasa kinaomboleza kifo cha mwanachama wake mkuu Abdhul Bare Juma.

 

Juma ameaga dunia hii leo alfajiri nyumbani kwake mtaa wa Ganjoni.

Mwendazake amewahi kuhudumu kama Mwenyekiti wa Arena katika maonyesho ya Mombasa pamoja na kuwa mwekahazina katika shirikisho la soka tawi la Mombasa FKF chini ya mwenyekiti Gabriel Mgendi.

Hapa sauti ya pwani Abdhul Bare Juma alikuwa mchangiaji na msikilizaji mkubwa.

Kutoka kwetu kama idhaa tunaitakia familia nguvu wakati huu mgumu wa maombolezi.

Comment here