AfyaKimataifa

Athari za Saratani nchini

Imebainika kwamba takriban watu elfu 30 hufariki dunia kila mwaka humu nchini kutokana na maradhi ya saratani.

Kulingana na ripoti ya benki ya dunia, saratani ya kizazi inaongoza kwa visa vipya kwa asilimia 11, ikufuatwa na saratani ya matiti kwa asilimia 10, kisha saratani ya ngozi ya njia ya kibofu ikiwa na asilimia 6.

Katika mahojiano ya kipekee na kituo kimoja cha radio,  Amina Habib mtaalamu wa tiba ya maradhi ya saratani ameweka wazi kuwa ugonjwa wa

saratani ni moja ya maradhi ambayo yameathiri wengi ulimwenguni huku akisema saratani ya matiti akiitaja kuathiri idadi kubwa ulimweguni.

Daktari Amina anasema utafiti bado unafanywa kuchunguza ni kwa nini kaunti ya Kilifi imeathirika sana na saratani ya sehemu ya mfereji wa chakula ambao unaunganisha koo na tumbo.

Ikumbukwe kuwa watu milioni kumi hufariki kila mwaka ulimwenguni kutokana na maradhi ya saratani

Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni kukinga, kutoa msaada, kuhamasisha na kuwa na mshikamano.

Comment here