Siasa

Shughuli ya kukusanya maoni kutoka kwa umma kuhusu BBI kuanza alhamisi hii mjini Mombasa.

Shughuli ya kukusanya maoni kutoka kwa umma kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020 kupitia BBI inatarajiwa kuanza alhamisi hii hapa mjini Mombasa.

Shughuli hiyo imepangwa kutekelezwa kwa muda wa siku mbili katika maeneo bunge yote sita ya kaunti ya Mombasa.

Kulingana na ilani ya bunge la kaunti ya Mombasa, siku ya alhamisi wakaazi wa eneo bunge la Kisauni, Nyali na Mvita watapata fursa ya kutoa maoni huku ijumaa ikiwa ni zamu ya wakaazi wa Likoni, Changamwe na Jomvu.

Katika eneo bunge la Kisauni zoezi la kukusanya maoni litafanywa katika uwanja wa cobra, huku eneo bunge la Nyali zoezi hilo likitarajiwa kufanywa katika uwanja wa Frere town huku wakaazi wa Mvita wakitarajiwa kukusanyika katika ukumbi wa Tononoka kutoa maoni yao.

Huku likoni itakuwa katika uwanja wa Likoni Stadium, Changamwe katika ukumbi wa Changamwe na hatimae jomvu katika uwanja wa aldina visram.

Ukusanyaji huo wa maoni unatekelezwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana.

Na:Warda Ahmed

Comment here