Habari

Wawakilishi wadi kaunti ya Taita Taveta sasa wanataka majibu kuhusu shughli ya malipo kwa wafugaji

Wawakilishi wadi kaunti ya Taita Taveta sasa wanataka majibu kuhusu shughli ya malipo kwa wafugaji sawa na wakulima ambao mifugo wao wameliwa na simba eneo la Maktau huko Mwatate.

Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Bura, Patel Mn’gambwa wawakilshi hao wanasema sharti shirika la KWS lionyeshe nia ya kufidia wakulima sawa na wafugaji eneo hilo.

Haya yanajiri huku wafugaji eneo hilo wakikadiria hasara kila mara kufuatia mifugo kuvamiwa na simba kutoka mbuga ya Tsavo Magharibi.

NA:FATUMA RASHID

Comment here