AfyaHabari

Sekta ya kilimo yaimaria zaidi huko Jilore

Sekta ya kilimo imeimarika hata zaidi kule Jilore eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi baada ya serikali ya kaunti hiyo kutoa Pembejeo pamoja na mifugo kwa wakaazi eneo hilo.

Kulingana na mwakilishi wa wadi hiyo Daniel Chai Chiriba hatua hiyo huenda ikaimarisha usalama wa chakula eneo hilo na kupiga jeki wenyeji waliokuwa wakihangakia familia zao.

Chiriba anayetambulika kama Bonyeza, anasema zaidi ya mabomba hamsini tayari yamesambazwa kwa wakulima mbali mbali eneo hili ili kuwawezesha kunyunyizia maji mimea yao.

Anasema japo kwa sasa serikali ya kaunti hiyo imesambaza maji safi sehemu mbali mbali wadi hiyo chini ya uongozi wake, yapo maeneo machache yanayohitaji kupigwa jeki na serikali hiyo.