HabariKimataifa

Rais Kenyatta achaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa muungano wa mataifa ya Afrika Mashariki

Rais Uhuru Kenyatta amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa muungano wa mataifa ya Afrika Mashariki.

Rais Kenyatta amechukuwa wadhfa huo kutoka kwa rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye amehudumu tangu mwaka 2019.

Wakati huo huo Peter Mutuku Mathuki wa Kenya ndiye katibu mkuu mpya wa muungano huo.

Mutuku ameteuliwa wakati wa kongamano la marais wa Afrika Mashariki ambalo limefanyika hii leo ambapo atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.