Habari

Wakenya wahimizwa kujibu jumbe za huduma namba wanazotumiwa

Imebainika kwamba ni watu elfu 300 pekee waliojibu ujumbe kuhusu ni wapi wanataka kadi zao za huduma zitumwe kati ya watu milioni 2.6 waliotumiwa ujumbe huo kupitia simu zao.

Akiongea katika kipindi cha baraza letu hapa sauti ya Pwani, msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amewahimiza wakenya kutopuuza ujumbe wanaotumiwa ambao unawahitaji kujibu na kueleza ni wapi wangependa watumiwe kadi zao.

Wakati huo huo amesema wana matumaini kwamba kufikia mwisho wa mwaka huu wakenya milioni 37 waliosajiliwa kupata huduma namba watakuwa wamepata kadi hizo na wataanza kuzitumia kwa kila huduma ya serikali.