AfyaHabari

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema chanjo dhidi ya virusi vya corona itawasilishwa nchini siku ya jumanne wiki ijayo.

Akizungumza kaunti ya Nyeri, Kagwe amesema wahudumu wa afya watapewa kipaumbele katika chanjo hiyo, kisha baadaye maafisa wa usalama, walimu na wafanyakazi wengine wanaotangamana na umma katika majukumu yao ya kazi.

Kagwe amesema chanjo hiyo kuwasilishwa nchini haimaanishi wakenya wanafaa kuacha kuzingatia masharti ya wizara ya afya ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona.

Waziri kagwe amesema visa vya Covid 19 vingali juu nchini na kunahitajika umakinifu kutoka kila mwananchi.