HabariSiasa

Naibu rais Dakta William Ruto anasema kamwe hatakubali azma yake kumrithi rais Uhuru kenyatta kuzamishwa na baadhi ya wanasiasa nchini.

Akizungumza eneo la Gatura Gatanga kaunti ya Murang’a Ruto amepuuzilia mbali wanasiasa wanaohjaribu kutatiza amza yake akisema hilo halitafaulu.

Wakati huo huo ameshikilia kuendelea na mpango wake wa kipiga jeki kifedha wananchi wa pato la chini licha ya pingamizi kutoka baadhi ya viongozi nchini.