HabariKimataifa

Polisi nchini Myanmar imewafyatulia risasi waandamaji.

Leo ikiwa ni siku mbaya kabisa ya umwagaji damu tangu maandamano yalipoanza wiki kadhaa zilizopita dhidi ya mapinduzi ya kijeshi.Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani ukandamizaji unaofanywa dhidi ya waandamanaji ikisema watu 18 wameuawa leo.

Afisa wa Umoja wa Maatifa ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema ofisi hiyo imethibitisha karibu vifo vya watu watano mjini Yangon.

Gazeti la Myanmar Now limeripoti kuwa watu wawili wameuawa katika mji wa pili wa Mandalay.