Habari

Kamishena wa kaunti ya Kwale Joseph Kanyiri amewaonya wazazi wa kaunti hiyo dhidi ya kujihusisha na visa vya ndoa za mapema.

Akizungumza katika eneo la Diani, Kanyiri amesema wazazi watakaopatikana wakiwaozesha wasichana wao wa umri mdogo watakabiliwa kisheria.

Vile vile, kamishena huyo ameonya wale wanaohusika na visa vya kuwaoza watoto wa kike watashtakiwa mahakamani.

Wakati huo huo, Kanyiri amewaonya wakaazi dhidi ya visa vya ulanguzi wa watoto kwa kigezo cha kuwatafutia ajira katika mataifa ya nje.

Kiongozi huyo amesema hatua hiyo inakiuka haki za watoto wanaohadaiwa na kuingizwa katika makundi ya uhalifu.

 

NA BINTI KHAMISI