HabariSiasa

Spika wa bunge la kaunti ya kilifi Jimmy Kahindi anasema Idadi kubwa ya wakaazi kaunti hiyo hawajasoma na kuelewa kilichomo ndani ya ripoti ya mswada wa BBI.

Kulingana na Kahindi hayo yalibainika wakati wa vikao vya kuchukua maoni ya wananchi kuhusu BBI kutokana na  maswali waliyopata kutoka baadhi ya wakaazi.

Kahindi anasema huenda hatua hiyo inachangiwa na wanasiasa wanaowahadaa wakaazi nyanjani kuhusu umhimu wa mswada huo.

Wakati huo huo Spika huyo amewataka viongozi kukoma kuwahadaa wakaazi akipigia upato ripoti hiyo kuwa uchumi wa baharini na masuala mengine ya pwani yako kwenye ripoti hiyo.

Mwisho.

 

Na Joseph Yeri