AfyaHabariMombasa

Wasichana walio na umri mdogo eneo la changamwe hapa Mombasa wamenufaika na msaada wa vitambaa vya sodo kutoka kwa wakfu wa Omboko.

Mwanzilishi wa wakfu huo, Dennis Omboko amesema kuwa janga la korona lilisababisha wazazi wengi kukosa ajira hivyo imekuwa vigumu wengi wao kuwa na uwezo wa kuwanunulia sodo wanawao.

Omboko ameongeza kwamba zoezi hilo la ugavi wa sodo litahusisha hamasa kwa wasichana hao kuhusu namna ya kujiweka salama.

Amekariri kuwa baadhi ya wasichana wako hatarini kutokana na mitego ya wanaume waliokosa utu.