Habari

Serikali ya kaunti ya Kilifi inapania kuimarisha miundomsingi katika wadi ya Kakuyuni eneo bunge la Malindi.

Kulingana na mwakilishi wa wadi hiyo Nixon Mramba zaidi ya barabara saba wadi hiyo zitakarabatiwa kwa kima cha shilingi milioni 20 katika bajeti ya mwaka huu wa kifedha.

Mramba anasema serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 4 kujenga vivuli kwa wahudumu wa pikipiki wadi hiyo katika bajeti hiyo.

Wakati huo huo kiongozi huyo amewarai wakaazi wadi hiyo kuunga mkono juhudi za marekebisho ya katiba zinazoendelea kwa sasa akisema hatua hiyo itaongeza kiwango cha miradi nyanjani.

Amesema kwa sasa idadi ya miradi inayofika nyanjani ni michache mno akiwataka wenyeji kupitisha marekebisho hayo wakati wa kura ya maamuzi.