Akiongea na wanahabari baada ya kukamilisha kikao hicho gavana wa kaunti hii Salim Mvurya amesema hali hio imetokana na hofu mpya ya msambao wa homa hio ikizingatiwa kaunti ya Kwale imepakana na taifa jirani la Tanzania.
Mvurya amewarai wananchi kuzingatia Masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ili kuepuka maambukizi.
Ni kauli iliyoungwa mkono na kamishna wa kaunti hio Joseph Kanyiri akisema idara ya usalama haitaruhusu mtu yeyote kuingia katika kaunti bila kupimwa.
Na Binti Khamis.