HabariMazingira

Wakaazi wa Tana Delta kaunti ya Tana River wameombwa kutoendeleza shughuli za kilimo katika maeneo ambayo ni njia za wanayamapori ili kuepuka uhasama kati ya wanyama hao na binadamu.

Ali Tambo mwanakamati wa uhifadhi wa mazingira na utoaji fidiaji kwa walioathirika na mashambulizi wa wanyamapori eneo la Tana Delta, amesema wanyama pori wameelekea sehemu ya chini kutafuta maji kutokana na hali ya kiangazi inayoshuhudiwa kaunti ya Tana River.

Tambo amewarai wakaazi kupiga ripoti kwa shirika la KWS kabla ya masaa 24 kupita ili waweze kupata fidia na hatua ya haraka kuchukuliwa kuzuia wanyama hao kuleta madhara Zaidi.

ameomba ushirikiano kati ya wakaazi idara ya KWS na walinda mazingira ili visa vya uvamizi kutoka kwa wanayamapori viweze kukabiliwa.

Haya yanajiri siku chache tu baada kisa ambapo wakulima wawili walijeruhiwa na mmoja kupoteza maisha huko Tarasaa baada ya kuvamiwa na fisi shambani.

Na Guracho Salad