HabariSiasa

Viti vya maeneo bunge ya Bonchari na Juja vyatangazwa kuwa wazi…

Spika wa bunge la Kitaifa Justin Muturi ametangaza kuwa wazi kwa viti vya maeneo bunge ya Bonchari na Juja.

Kiti cha eneo bunge la Bonchari kiliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge John Oroo Oyioka aliyefariki Februari 15 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kiti cha eneo bunge la Juja pia kilisalia wazi kutokana na kifo cha mbunge Francis Munyua Waititu. Wakapee kwa jina la utani alifariki Februari 22, katika hospitali ya MP Shah.

Alikuwa ameugua saratani ya ubongo kwa muda mrefu.