HabariSiasa

Rais afutilia mbali mkutano wa kuadhimisha miaka mitatu ya HANDSHAKE………

Rais Uhuru Kenyatta amelazimika kufutilia mbali mkutano wa kuadhimisha miaka mitatu ya mapatano kati yake na kinara wa ODM Raila Odinga maarufu Handshake.

Rais Kenyatta na Odinga walitarajiwa kutoa muongozo ya jinsi watavyoendesha kampeni ya marekebisho ya katiba kupitia BBI.

Ratiba ya viongozi watakaoendesha kampeni hiyo ingetolewa wakati wa mkutano huo katika Ikulu jijini Nairobi.

Inaarifiwa kwamba rais amechukua hatua hiyo kutokana na mashinikizo ya odm kwamba fedha zitengwa ili kufadhili kampeni huku ikiarifiwa kwamba tofauti kati yake na Odinga ambapo kulingana na wandani wa rais wanapanga kutumia mchakato huo kujipigia debe.

Hata hivyo kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya amesema rais amefanya hivyo ili kuyaruhusu mabunge yote kujadili mswada wa marekebisho ya katiba.