HabariMazingira

Mashirika ya kijamii yatishia kuishtaki serikali ya Mombasa…..

Mashirika ya kutetea haki za binadamu sasa yametishia kuishtaki serikali ya kaunti kwa kuwafurusha wakaazi  wa Buxton hapa Mombasa kiholela na bila ya kufuata sheria ipasavyo huku baadhi ya wakaazi wakiachwa njia panda.

Wakiongozwa na Johnpaul OBONYO wa shirika la haki yetu anyesimamia masuala ya ardhi, wanaharakati hao wanasema serikali imeendesha zoezi hilo kwa haraka mno ikizingatiwa kwamba kuna wanafunzi ambao wanaishi kwenye makaazi hayo na wanatarajiwa kufanya mitihani ya kitaifa.

Mashirika hayo sasa yanamlaumu gavana wa Mombasa kwa kutosema ukweli kuhusiana na mradi huo wa Buxton  huku wakisema wakaazi hao wamepewa muda mchache mno kuondoka kwenye makaazi hayo ili kupisha ubomozi.

Gabriel Dolan ni mkurugenzi mkuu wa shirika la haki yetu.

Ikubukwe kwamba zaidi ya familia 500 zimeondolewa eneo hilo ili kupisha ujenzi wa mradi huo ambapo wamelipwa jumla ya shilling elfu 240.