HabariSiasa

Mwashetani atofautiana vikali na Zulekha Hassan…..

Mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani ametofautiana vikali na mwakilishi wa kike wa kaunti ya Kwale Zulekha Hassan kuhusu suala la mzozo wa ardhi katika kaunti hiyo.

Mwashetani amemshtumu Zulekha kwa madai ya kumuingilia kuhusu jinsi anavyolishughulikia suala la utatuzi wa mzozo wa ardhi.

Mbunge huyo amemtaka Zulekha kutafuta suluhu ya matatizo yanayowakumba wananchi badala ya kuwakosoa viongozi wenzake.

Mwashetani ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa kamati ya ardhi bungeni amejitetea kuwa suala la ardhi linatatuliwa kwa kuzingatia utaratibu wa sheria zilizowekwa.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Zulekha kupinga vikali azma ya Mwashetani ya kuwania kiti cha ugavana wa Kwale mwaka ujao.