AfyaHabari

Curfew yaongezwa muda, huku mikutano ya kisiasa ikipigwa marufuku…..

Rais Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa marufuku ya kutotoka nje maarufu kafyu kwa muda wa siku 60 zijazo.

Akihutubia taifa kuhusiana na mikakati ya covid 19, rais Kenyatta amesema wale ambao wanafanya kazi masaa hayo ya kafyu hawataathirika na agizo hilo.

Wakati huo huo amesema mikahawa na sehemu za burudani zitasalia kufungwa ifikapo saa tatu usiku.

Wakati huo huo rais Kenyatta ametangaza kwamba mikutano yote ya kisiasa imepigwa marufuku kwa muda wa siku 30 zijazo.

Amewahimiza maafisa wa polisi kutumia jukumu lao katika kuhakikisha sheria inafuatwa.
wakati huo huo rais Kenyatta ameamuru kwamba shughuli za mazishi kufanywa ndani ya masaa 72 baada ya mtu kufariki kutokana na covid 19 huku watakaohudhuria wasizidi watu 100.

Pia ameagiza wanaohudhuria shughuli za harusi wasizidi watu 100.

Kulingana na rais Kenyatta kiwango cha maambukizi kufikia mwezi January kilikuwa asilimia 2, lakini kufikia mwezi huu wa machi kimefikia asilimia 13 na kinaendelea kupanda zaidi.

Haya yanajiri huku Kenya ikiingia katika awamu ya tatu la maambukizi.