Habari

Atakayekiuka sheria za kukabili corona kukamatwa bila ya kujali cheo chake…

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria wote wanaokiuka sheria za kukabili maambukizi ya covd 19 bila kujali cheo akiwepon yeye mwenyewe.

Akihutubia taifa, rais Kenyatta amesema taifa haliwezi kuendelea kuhatarisha maisha ya wakenya kutokana na virusi vya korona ambavyo vimesababisha maafa mengi ulimwenguni kote.

Kiongozi wa taifa amesema iwapo taifa lisingechukua tahadhari ya kulinda raia wake, kwa sasa idadi ya maambukizi ingefikia Zaidi ya milioni nchini.

Wakati huo huo amesema kunamatumaini ya uchumi wa nchi unaimarika japo amekumbusha wakenya kujilinda na kufuata masharti ya kukabili maambukizi ya virusi vya corona.

Ameongeza kuwa siku zahivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la maabukizi nchini jambo linalochangia serikali kuweka makataa Zaidi.

Kwa upande wake Gavana wa embu ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la magavana nchini, amesema atashirikiana na magavana kote nchini kutelekeza masharti ya kupambana na maambukizi ya virusi ili kulinda wakenya.