HabariMombasaSiasa

Kamati ya uangalizi wa wanawake Mombasa yapinga BBI…

Mombasa imeapa kutounga mkono ripoti ya BBI ikidai itaongeza gharama ya maisha kwa mwananchi Kamati ya kitaifa kuhusu uangalizi wa wanawake tawi la wa wakaida.

Wakiongozwa na Feni Katana mwanachama wa kamati hiyo anasema kwa sasa taifa linamadeni mengi na ripoti hiyo imeongeza sehemu za uwalikishi pamoja na idadi ya viongozi hatua ambayo inakuja na matumizi mengi ya fedha kupitia ushuru wa mwananchi.

Anasema serikali inafaa kuangazia mawasla muhimu yanayokumba taifa kwa sasa ikiwepo kuangazia kufufua uchumi n ahata kupambana na maabukizi ya virusi vya Corona.

Kulingana na Joyce Dama mwanachama wa kamati hiyo, katiba ya sasa inavipengee vingin ambavyo havijatekelezwa kwa sasa, na huenda ni mzaha kuifanyia marekebisho katiba hiyo.

Ametoa mfano swala la ardhi ambalo limekuwa na athari kubwa hapa Pwani akidai ripoti ya BBI haijaangazia wazi namna itakavyoshughulikia swala hilo.