HabariMombasa

Watu kadhaa wakamatwa katika oparesheni ya dawa za kulevya MOMBASA…

Zaidi ya watu 30 wamekamatwa huku ma elfu ya lita ya pombe haramu yakimwagwa katika maeneo mbali mbali ya kaunti ya Mombasa kufuatia oparesheni dhidi ya dawa za kulevya na pombe haramu iliozunduliwa wiki hii.
Katika oparesheni hio iliofanyika maeneo yote Mombasa pombe aina ya chang’aa, mnazi na kang’ara zilinaswa na kuharibiwa huku maskani zaidi ya tano zikiharibiwa katika maskani ya kuuza pombe hizo haramu.
Akidhibitisha kamishna wa Mombasa Gilbert Kitio amesema kuwa wanasaka baadhi ya wenye maskani hizo ambao walitoroka wakati wa oparesheni.
Aidha misukuto zaidi ya kumi ya bangi ilipatikani katika maskani hizo. Kitio amesisitizi kuwa oparesheni itaendelezwa kwa wiki mbili ili kuwatafuta wahusika waliochangia katika utumizi wa mihadaratina kumaliza matumizi ya dawa hizi.
Idara mbalimbali ikiwemo polisi, machifu mamalaka ya kupambana ma dawa za kulevya nchini Kenya NACADA vilevile iliweza kuhusika katika oparesheni hio.