Habari

Serikali iwekeze katika utafiti ili kukabili uhalifu,asema Matiang’i…

Waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi amesisitiza haja ya kuwekeza zaidi katika utafiti ili kukabili visa vya uhalifu humu nchini.

Akizungumza katika hafla ya kufuzu kwa waendesha mashtaka 48 jijini Nairobi, Matiangi anasema serikali inendelea kuwekeza katika mikakati ya kushirikiana na idara mbali mbali ili kuimarisha usalama wa kitaifa.

Naye mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin HAJI  amewahimiza maafisa waliofuzu kutekeleza majukumu yao bila ya mapendeleo.