AfyaHabari

Wadau wa Utalii wahimiza serikali kuwapa chanjo ya Covid 19.

Wadau Katika sekta ya utalii hapa Pwani wanasema wanamatumaini makubwa ya idadi ya watalii kuongezeka msimu wa sherehe za pasaka.

Wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano wa wamiliki wa mahoteli Sam Ikwae, wadau hao vile vile wamesema sheria za kudhibiti maambukizi ya corona nchni zimekuwa na athiri pakubwa katika sekta hiyo.

Ikwae amesema masharti hayo yamekuja na gharama kubwa hasa upande wa usafiri wa utalii.

Kuhusu chanjo ya Covid 19 Ikwae amesema serikali inafaa kuangazia kuwapa chanjo hiyo wahudumu wa sekta ya kitalii kama njia ya kuongeza ujasiri miongoni mwa wafanyakazi na watalii.