AfyaHabari

WAHUDUMU WA AFYA LAMU WAPEWA CHANJO YA COVID 19.

Kaunti ya Lamu imeanza zoezi la kuwachanja wahudumu wa afya dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri wa afya wa kaunti ya Lamu Ann Gathoni amesema kaunti ya Lamu imepata dozi 1,500 za chanjo hiyo kutoka serikali ya kitaifa, ambapo wahudumu wa afya 897 wa kaunti hiyo ndio wamepewa kipaumbele katika awamu ya kwanza ya utoaji wa chanjo hiyo.

Gathoni amesema chanjo hiyo itatolewa katika hospitali kuu wa King Fahad, hospitali ya Faza na ile ya Mpeketoni na serikali iko na mpango wa kusambaza chanjo hiyo mashinani ili kuwafikia wananchi.

Waziri huyo amesema chanjo hiyo ni salama na hakuna haja ya watu kuwa na uoga huku akitoa wito kwa wakaazi wa Lamu na Wakenya wote kwa jumla kuwa tayari kupokea chanjo hiyo kwa ajili ya kulinda afya zao

By Guracho Salad.