HabariKimataifa

Rais Kenyatta amuomboleza rais Magufuli.

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi rambi Kwa raia wa Tanzania kufuatia kifo cha rais wa Taifa hilo John Pombe magufuli aliaga dunia jana Jumatano.

Akizungumza Jijini Nairobi rais Kenyatta amesema afrika mashariki na bara afrika kwa jumla wanaomboleza na raia wa Tanzania kutokana na umoja ambao umedhihirishwa baina ya nchi wanachama.

Rais Kenyatta amemtaja Mgufuli kama rafiki na kiongozi aliyejitolea kuhudumia raia wake kwa ukakamavu.

Amesema Kenya itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maswala mbali mbali ya maendeleo.

Wakati huo huo Kiongozi wa taifa ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ametangaza bendera ya jumuiya hiyo na ya Kenya kupeperushwa nusu mlingoti hadi jioni ya siku ambayo Magufuli atazikwa..

Mwisho

By. Jira